Monday, September 15, 2014

Wafanyakazi wa benki ya NBC wajimwagia maji baridi kuchangiha fedha kupambana na Ugonjwa wa Fistula

Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Flora Lupembe (kulia) akimwagiwa maji baridi na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rukia Mtingwa katika hafla ya kumwagiana maji baridi iitwayo ‘Ice Bucket Challenge’ yenye makusudi ya kuchangisha fedha kwa ajili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mhazini Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Ivan Tarimo (kushoto) akimwagiwa maji baridi na mmoja wa mfanyakazi mwenzake katika hafla ya kumwagiana maji baridi iitwayo ‘Ice Bucket Challenge’ yenye makusudi ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Mussa Jallow (katikati) naye akimwagiwa maji baridi ili kutimiza azma ya benki hiyo katika kutafuta fedha ili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa fistula nchini.


Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Binafsi na biashara ndogondogo na za kati, Isidori Msaki (katikati) akijitahidi kujizuia wakati wafanyakazi wenzake wakimmwagia ndoo za maji baridi katika hafla hiyo.
kaimu ofisa mwendeshaji mkuu wa benki ya nbc, Jamie Loden akijimwagia maji baradi ili kusaidia harakati za benki hiyo kuchangisha fedha katika tukio hilo liitwalo ‘Ice Bucket Challenge’ kusaidia wanawake wanaokabiliwa na ugonjwa wa fistula. Kiasi cha fedha kitakachopatika kitapelekwa katika Hospitali ya CCBRT kwa madhumuni hayo.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Jaffari Matundu (kushoto) akimwagiwa maji na mfanyakazi mwenzake katika tukio la Ice Bucket Challenge lenye lengo la kukusanya fedha kusaidia wanawake wanaosumbulia na ugonjwa wa fistula.
Unaweza kuona kama mzaha Fulani lakini ndivyo ilivyokuwa kwa maofisa hawa wa NBC walipoamua kushiriki tukio la ‘Ice Bucket Challenge’ na kumwagiana maji baridi ili kuchangisha fedha kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula nchini.

Related Posts:

  • It Is Accolades to Generous America IT was all smiles among the education sector fraternity on Tuesday when the nation received a generous donation of 2,500,000 science text books from the United States of America. Indeed, the donation is a heartfelt gestu… Read More
  • Benki ya Exim yakarabati kituo cha watoto wenye ulemavu Morogoro Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Morogoro, Bi Anna Wesiwasi (wapili kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi wa Kituo cha Amani cha watoto wenye ulemavu, Padri Beatus Sewando (watatu kulia) mara tu baada ya kuzindua jengo la ki… Read More
  • Washington set to boost EAC trade The United States says it will support the East African Community (EAC) to overcome trade barriers and improve competitiveness of its export products in the international markets. This follows a Cooperation Agreemen… Read More
  • Poor Children Increasing Not many people know that enlisting child labour is a crime that attracts a one-year jail term or heavy fine. Most child labourers are made to toil for hours in the hot sun, many of them on empty stomachs. The meagre earni… Read More
  • Dar Charity Goat Races launches in Dar today Southern Sun Hotel Sales Manager, Punim Kanabar (2nd L) speaking to journalists on her hotel sponsorship towards this year Dar Charity Goat Races scheduled for May 30th this year in Dar es Salaam. It wa… Read More

0 comments:

Post a Comment