Friday, September 12, 2014

AMREF NA KCB ZASHIRIKIANA KATIKA ELIMU ZA WAKUNGA‏

Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania (kushoto)Moezz Mir akimsikiliza kwa makini  Mkurugenzi Mkazi wa  Amref Heath Africa Tanzania Dk. Festus Ilako,  jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akiongerea  juu ya ushirikiano wao na benki hiyo  katika kusaidia suala zima la Afya ya mama na mtoto nchini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania (kushoto)Moezz Mir  akimkabidhi  Mkurugenzi Mkazi wa  Amref Heath Africa Tanzania Dk. Festus Ilako,  hundi yenye thamani ya shilingi milioni 48. Kwa ajili ya kuwasomesha wakunga 10 ambao baada ya kupata elimu wataajiriwa katika vituo vya afya hasa vijijini ili kuwasaidia akinamama wanaohitaji huduma za uzazi.KCB na AMREF wametangaza ushirikiano  katika kusaidia suala zima la Afya ya mama na mtoto nchini, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, wapili kutoka kushoto ni  Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB  Christina Manyenye na Meneja msimaizi wa mifuko wa jamii  wa Amref Lilian Nsemwa.( fund Raising Manager)



 Mkurugenzi Mkazi wa  Amref Heath Africa Tanzania Dk. Festus Ilako,  akisisitiza jambo  kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawapo pichani)wakati alipokuwa akiongelea  juu ya ushirikiano wao na benki KCB Tanzania  katika kusaidia suala zima la Afya ya mama na motto nchini .Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Moezz Mir   na Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB  Christina Manyenye wakimsikiza  kwa makini.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania Moezz Mir   akiongele juu ya ushirikiano wao na Amref Heath Africa Tanzania  katika kusaidia suala zima la Afya ya mama na motto nchini Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa  Amref Heath Africa Tanzania Dk. Festus Ilako,   na Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB  Christina Manyenye

0 comments:

Post a Comment